GET /api/v0.1/hansard/entries/1353596/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1353596,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353596/?format=api",
    "text_counter": 462,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Molo, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
    "speaker": null,
    "content": "katika sehemu ambazo ziko na bahari, kama kule Lamu na Mombasa, utangamano kati yao na hao wanyama pori uweze kuzingatiwa ili tuweze kuzizuia hizi ajali. Nawahimiza wahusika wote ambao wanalinda wanyama pori, haswa hao ambao wanakaa karibu na mito, kuhusisha jamii ambazo zinaishi katika hayo maeneo. Mara nyingi kutafuta watu kwengine kulinda wale wanyama pori ilhali kama tungeweza kuwachukua wale wanaoishi pale, wangeweza kufanya kazi bora zaidi. Kwa mfano, maafisa wa kulinda misitu walichukuliwa juzi. Natumai kwamba wale ambao watachukuliwa baadaye ni wale wanaokaa karibu na misitu kwa sababu wao ndiye wanauelewa, wameishi karibu na hiyo misitu kwa muda mrefu na hata wengine wanaweza kuwaongelesha wanyama wengine wa porini. Wamaasai wengine wanapitana na simba hivi hivi tu na wanaelewana lugha. Lakini ukinichukua mimi kutoka Molo niende niwe askari wa kulinda simba, pengine nikimwona simba ametokea, jambo ambalo nafikiria la kwanza ni kumpiga risasi. Sio vile ambavyo tunaweza tangamana. Kwa hivyo, nahimiza tuzingatie wale ambao tayari wanakaa kati ya wanyama pori kuawalinda kwa sababu wataweza kufanya kazi bora zaidi kuliko hao wengine. Hongera kwa Mswada huu mzuri na nauunga mkono. Asante Mhe. Spika wa Muda."
}