GET /api/v0.1/hansard/entries/1353606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1353606,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353606/?format=api",
    "text_counter": 472,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii kuunga mkono Mswada ulioletwa katika Bunge hili na Mhe. Ruweida kutoka kule Lamu Mashariki. Kwanza, ningependa kumpatia dadangu Mhe. Ruweida kongole kwa kuweza kufikiria na kuona kuwa wakaazi wa Pwani wanaangamia. Pwani ni sehemu ambayo imepuuziliwa mbali pakubwa sana kwa miaka mingi. Ndio maana kila siku wanalia wakisema ‘Pwani si Kenya’. Tunaweza kupinga maneno haya kama viongozi lakini mwisho tunayapiga msasa na kuyakubali. Uchumi wa Pwani unategemea bahari. Kama viongozi wangetilia maanani uchumi wa bahari, wakaazi wa Pwani wangeweza kulisha taifa hili kwa jumla. Wapwani wana uwezo wa kuleta mapato ya kulisha taifa lote la Kenya. Hoja hii ni kwamba mkaazi wa Pwani anategemea kwenda baharini kufanya uvuvi lakini iwapo atapata ajali ama kuumwa na samaki walio baharini, hatambuliwi wala kudhaminiwa. Bahari lile ni kubwa. Sio ziwa. Lina viumbe vingi vya maana kama nyangumi, papa, taa, samaki wa mawe, pweza, ngisi, tafi na changu. Kuna samaki ambaye ni kitoweo lakini akikuuma ana sumu ambayo inaweza kuharibu viungo vya mwili kama roho. Inaweza kumfanya mtu kupooza mwili. Serikali bado haijaona umuhimu wa kuhakikisha usalama wa wavuvi baharini. Tunaomba Hoja hii iwekwe kama mabadilisho katika Mswada wa sheria ya wanyama pori ili kuongeza tija ya wavuvi. Wanapoumia baharini, wapate malipo. Hivi karibuni nilimskia Rais akitangaza kuwa angependa kupeleka Wakenya katika mataifa ya nje ili wapate kazi. Hii ni kwa sababu Wakenya hawajajua thamani ya Bahari Hindi la Kenya. Likitambuliwa na kuthaminiwa, litaweza kulisha taifa hili. Bahari hili limenyooka kutoka Lamu, Mombasa hadi Tanzania na lina viumbe wengi walio na thamani kubwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}