GET /api/v0.1/hansard/entries/1353648/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1353648,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353648/?format=api",
    "text_counter": 514,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Bwana Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Kwanza, nampongeza dada yetu, Mhe. Captain Ruweida, kwa kuleta Mswada huu. Ni ajabu kuwa kwa muda mrefu sana, hatukufikiria kuwa kama vile watu uuawa na ndovu au kuuliwa na simba, basi watu wa pwani pia wako na simba na ndovu wao baharini. Nazungumza nikijua kuwa nina wavuvi katika eneo Bunge langu la Matuga kuanzia Likoni, Ng’ombeni, Tiwi, Waa na sehemu nyinginezo. Watu hao hutegemea uvuvi na bahari ili kujikimu kimaisha. La ajabu ni kuwa ni kupitia Mswada huu sasa ndio wataweza kupata fidia iwapo watapambana na wanyama hatari wanapotafuta riziki baharini. Mnyama moja ambaye wengi wetu tukienda pwani hatukosi kunywa supu yake ni pweza. Sitaeleza ni kwa nini tunapenda supu yake, lakini pweza amepata umaarufu sana. Ukienda pwani na usinywe supu yake, basi labda hujafika pwani. Lakini wengi hawajui kuwa pia pweza ni hatari, haswa anapovuliwa. Yeye ni hatari hata kwa wapiga mbizi ambao humtafuta, na pia huvua aina zingine za samaki kama vile kamba na kamba-mti. Pweza anaweza kumfunga mpiga-mbizi kutumia mikono yake hadi ashindwe kuogelea. Hii inamaanisha kuwa hata uwe hodari wa kukaa chini ya maji dakika 10 au 15, unapozuiliwa pale ndani ya maji na pweza, unaweza kukosa hewa na kuaga dunia. Pia pweza ana ujuzi wa kutoa ile mikono yake na kuziba mvuvi pua. Ukizibwa pua, utachanganyikiwa na kukosa hewa, na hatimaye kuangamia majini. Waswahili husema, wavumao pwani ni papa, lakini wengi wamo. Ni kweli kuna wanyama wengi zaidi katika bahari mbali na hao ambao mwenye kuuleta Mswada huu amewataja. Mbali na papa, kuna bocho. Bocho ni aina ya samaki anayeweza kudhuru kila mtu. Unapotembea ufuoni mwa bahari, huwezi kumtambua. Kwani anafanana na jiwe na ana sumu kali sana. Kwa hivyo, mbali na wavuvi, ni hatari pia kwa yeyote ambaye anatembea sehemu ile. Ukimkanyaga na akudunge na kukutia ile sumu, unachukua muda mchache sana kupoteza maisha yako. Kuna samaki mwingine anayeitwa mkunga. Ni samaki na anavuliwa lakini anapokupata na kukukaribia vizuri na kugusa ngozi yako, inabambuka moja kwa moja. Inapobambuka, katika hali ya taharuki, unaweza kubaki majini upoteze maisha, na ukijiokoa, utakuwa na maumivu makali na vidonda hatari. Ni samaki ambao wangefaa kuorodheshwa katika nakala hii kama samaki hatari. Mtu akiweza kupambana nao, apewe ruzuku yake. Taa ni samaki mwingine hatari, kwani anaweza kumchapa mtu. Anapokuchapa, anakukata na kukupasua. Katika hali hii, taharuki hutokea na watu wanaweza kupoteza maisha yao. Mbali na samaki ambao nimewataja, kuna wengine kama chunusi, bunju na yavuyavu ambao ni hatari kwenye bahari. Katika kuhakikisha kwamba Mswada huu unakamilika, ipo haja ya kufanya marekebisho kuongeza hao samaki, kwa sababu wanapatikana katika ufuo wa kanda ya Bahari ya Hindi. Suala lingine ambalo linaenda zaidi ya Mswada huu ni muda ambao watu wanafaa kulipwa ruzuku. Je, ni wakati gani na ni hela ngapi? Katika sheria ambayo ipo kwa sasa, utapata kwamba mtu anapopoteza maisha, analipwa takriban shilingi elfu thelathini. Hii ni pesa finyu sana na haitoshelezi hata mtu kusema atagharamia kuitafuta. Licha ya kuwa inachukua muda mrefu, pia kuna zile taratibu za kutoa ripoti na kuona daktari. Katika hali hii, pengine kuwe na mazungumzo kwamba mtu anapoathiriwa na mnyama wa nchi kavu au samaki wa baharini, basi watolewe zile gharama za daktari; ajaziwe pesa ili apate matibabu kwa sababu sio kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}