GET /api/v0.1/hansard/entries/1353649/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1353649,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353649/?format=api",
"text_counter": 515,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "makusudio yake. Lakini labda mtu ni mvuvi na anatafuta riziki yake, au ni mtu anayetembea au kujivinjari katika sehemu hizi za Pwani. Kama watu wa Pwani ambao tunategemea bahari, Mswada huu umekuja wakati mwafaka, hasa katika ile azma yetu ya kuongeza utalii. Itakuwa muhimu watalii wakijua kwamba wanyama hatari baharini wanatambulika na kuorodheshwa kisheria, na kwamba endapo hatari itatokea, mbali na bima ambayo watakuwa wanaitumia, pia wanyama hao wanatambulika Kenya. Hili ni jambo ambalo litatuongezea katika sekta ya utalii. Wizara ya Madini na Uchumi Samawati imetilia mkazo sana jinsi tutaweza kunufaika na zile rasilimali za baharini. Mswada huu umekuja wakati mwafaka na utaweza kuendeleza azma hio. Wametoa boti, lakini ni zile ndogo ambazo ni wazi, na mara nyingi inabidi mvuvi ashuke. Tusisahau kwamba tuna uvuvi wa aina mbalimbali, nyavu na juya. Moja kwa moja, mtu analazimika kutoka kwa boti lake hata kama ana ile chombo, lakini aweze kushuka kwa maji ya bahari apige mbizi. Katika hali kama hizi, ndio watu wanakumbana na samaki hatari. Naunga mkono Mswada huu."
}