GET /api/v0.1/hansard/entries/1353963/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1353963,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353963/?format=api",
"text_counter": 242,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Kaunti ya Embu huwa tunalima miraa, muguka, avocado, kahawa na majani. Tumekubali kulima kabisa. Je, Bw. Waziri, unafikiria namna gani kuhusu kutujengea uwanja wa ndege ambao utasaidia kaunti za Embu, Tharaka-Nithi, Kirinyaga na pia upande wa Meru? Uwanja huu ukijengwa tutajivunia matunda ya Kenya Kwanza kwa kipindi cha miaka mitano. Pale kuna na uwanja wa ndege usiotumika. Kwa hivyo, kama Serikali ya Kenya Kwanza haina pesa, mnaweza kuturuhusu tutumie uwanja huo? Magari mengi yanayobeba miraa yamekuwa na shida kwa sababu ya kuuwa watu. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}