GET /api/v0.1/hansard/entries/1354322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354322,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354322/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe sauti yangu kwa Mswada wa kuidhinisha matumizi ya ziada ya fedha. Ninaunga mkono makadirio ambayo yameongezwa katika sekta ya elimu, usalama, afya na kilimo. Kilimo hasa ni muhimu kwa sababu ukulima ni uti wa mgongo wa taifa letu. Kwa sasa, hali ya taifa letu ni tata kwa sababu ya uchumi mbaya. Bajeti ya wakulima ikiongezewa itaongeza uzalishaji na uchumi utaboreka. Nina imani kuwa baadaye Rais wetu atapunguza zile kazi ambazo zimekuwa zikitujia sisi Wabunge kila wakati. Kwa upande mwingine, ile bajeti ambayo imeongezewa Ikulu na Ofisi ya Naibu Rais sio sawa. Hiyo bajeti ingeachwa vile ilivyo kwa sababu hata makadirio ya hapo awali yaliibua utata. Ni vyema kama ingepunguzwa na fedha hizo kuongezewa sekta ya afya, kilimo, usalama na elimu. Hiyo ni ishara ambayo itaguza na kutuliza nyoyo za wananchi wengi ambao wanahangaika kwa wakati huu na kumpatia Rais umaarufu zaidi katika uongozi wake. Kwa hivyo, ninaunga bajeti ya sehemu nne ambazo ni kilimo, usalama, elimu na afya. Lakini upande wa Ikulu, naomba radhi kwa sababu, kama Mama Kaunti, ninaona ni vyema ibaki ilivyo. Asante sana, Mhe. Spika."
}