GET /api/v0.1/hansard/entries/1354431/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354431,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354431/?format=api",
    "text_counter": 257,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Butere, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Nicholas Mwale",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Mwenyekiti. Ninasimama kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati kwa kuleta marekebisho haya. Alisisitiza umuhimu wa kufanya haya marekebisho alipoanzisha mjadala huu mara ya kwanza. Ninawaunga mkono Mwenyekiti wa Kamati na Mhe. wa Tinderet. Mwenyekiti wa Kamati ahakikishe kuwa pesa hizo zije kwa haraka mno ili Wabunge na Serikali kwa jumla waanze kuzingatia jinsi Wakenya wataishi maisha mema. Serikali ya Mheshimiwa William Ruto iliomba kura kwa kuongea kuhusu maneno ya mama mboga na vijana wa boda boda. Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi ambaye majina yetu yanafanana, Mhe. Ndindi, hajafafanua vizuri mbinu ambazo Serikali itatumia kuimarisha maisha ya mama mboga na vijana wa boda boda. Kwa hivyo, ndugu yangu Mwenyekiti, ninaomba uzingatie mama mboga na vijana wa boda boda katka bajeti ambayo itakuja huko mbeleni ili Serikali ifanye kazi jinsi ilivyoeleza wananchi."
}