GET /api/v0.1/hansard/entries/1354575/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354575,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354575/?format=api",
    "text_counter": 401,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nichangie Mswada huu. Mafuriko yametuathiri sana. Inasikitisha kuwa kila wakati tunapatikana ghafla. Ni muhimu tujitayarishe ili mafuriko haya yakija tena yapate tukiwa tayari. Siku nenda, siku rudi jambo ni lilelile. Pia, ningeomba kuwa isiwe ni lazima kila Mbunge aulize sawali kibinafsi, bali kila kinachonukuliwa hapa kigusie nchi nzima. Sio tu Lamu, Tana River na Garisssa kwa sababu jambo hili linaathiri sehemu nyingine pia. Tujadili tu Mswada huu kwa ujumla maanake maswali yatakuja mengi. Ni vyema tupate msaada kwa pamoja sote tulioathirika na mafuriko. Kwetu Lamu Mashariki kunasikitisha sana. Eneo lililoathirika sana ni Wadi ya Basuba. Kwa mfano, Shule ya Mangai iko upande wa pili wa mto. Sasa hivi, wanafunzi hawawezi kwenda Shule ya Mangai kwa sababu ya mafuriko. Watu wa Mararani wamefungiwa kabisa. Hawawezi kwenda Kiunga kwa sababu ya usalama na pia hawawezi kuvuka kwenda Mangai. Wamefungika kabisa na hawana pa kwenda. Kutoka Basuba hadi Milimani hakupitiki. Hata The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}