GET /api/v0.1/hansard/entries/1354576/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1354576,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354576/?format=api",
"text_counter": 402,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "piki piki hazipiti. Bodaboda tu ndio zimekuwa mbinu ya usafiri pekee eneo hilo kwa sababu ya kuwekwa kwa improvised explosive device (IEDs) barabarani. Alhamdulilahi, tunashukuru kuwa mambo ya kuwekewa vilipuzi barabarani hayasikiki tena kwa sababu ya mvua. Lakini sasa hatuna mbinu za usafiri. Sasa hivi, hakuna usafiri wa aina yoyote kutoka Basuba kwenda Milimani. Upande wa Kiangwi kwenda Basuba pia barabara imekatika. Watu wanaoweza kufikiwa sasa ni wale wa Kiangwi tu. Sehemu nyingine zote ni lazima jeshi liende lisaidie. Tunaomba Kenya Defence Forces (KDF) wasichoke kusaidia wakaazi hawa. Cha kusikitisha mno ni kuwa Lamu Mashariki haipo katika orodha. Ukipigia National DroughtManagement Authority (NDMA) wanasema tu Lamu Mashariki kuna mafuriko. Hawashughuliki kamwe. Hawana hata data. Red Cross wanashughulika tu sehemu zilizo na watu wengi. Kwa kuwa Lamu Mashariki watu ni wachache, hawashughulikiwi. Jambo hili linanisikitisha sana kama Mbunge wa kule."
}