GET /api/v0.1/hansard/entries/1354579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354579,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354579/?format=api",
    "text_counter": 405,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Wadi ya Basuba haiathiriki tu na mafuriko, siku zote wanalia maswala ya usalama. Kule ni matatizo zaidi. Nyumba za Basuba tunazijua. Wakaaji ni maskini na hata sijui kama wataweza kujenga tena bila msaada. Mafuriko yametuathiri. Ninaomba hatua za dharura zichukuliwe na Rais atangaze kuwa hili ni janga la kitaifa ili watu wapate msaada. Serikali ya kaunti inasaidia Lamu Magharibi tu. Haijafika Lamu Mashariki. Sijui mbona NDMA hawajafika pia. Nimewapigia simu na wanadai kuwa ni barabara tu imekatika na hakuna chochote wamefanya kusaidia. Sijui tukimbilie wapi sisi? Watu wanatutegemea na hatuna msaada wa kuwapatia. Sina mahali popote pa kutoa chakula cha msaada. Ninaomba sauti zetu zisikizwe. Donors pia wakumbuke watu wa Basuba na wasizingatie tu Lamu Magharibi. Lamu Magharibi imeathirika vilevile lakini Lamu Mashariki watu ni wanyonge zaidi."
}