GET /api/v0.1/hansard/entries/1354582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354582,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354582/?format=api",
    "text_counter": 408,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Asante sana, Bi Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia Mswada huu unaohusu janga la mafuriko. Ninaunga mkono kuwa mafuriko yatangazwe kuwa janga la kitaifa kwa sababu yameathiri wananchi pakubwa. La kusikitisha ni kuwa wananchi hawakutayarishwa sawasawa. Kulitangazwa kuwa El Nino ingekuja lakini baadaye tangazo hilo likakanushwa kufikia viongozi kuomba msahama kwenye runinga. Wananchi walitulia wakijua kuwa hali ni shwari. Ghafla bin vu, mvua ikanyesha usiku kucha na kusomba mifugo na vyakula. Watu wameathirika pakubwa. Eneo Bunge la Kisauni limeathirika pakubwa na mafuriko haya. Wadi saba ninazowakilisha zimekumbwa na mafuriko. Vyakula vimesombwa na maji na nguo zimebebwa. Watoto hawana makazi. Hali imekuwa ngumu. Watu hawa wanahitaji msaaada mkubwa. Serikali inapaswa kuwapatia chakula cha kutosha. Sio tu watu kupangishwa foleni na kupewa kilo mbili. Kilo mbili zitasaidia nini? Watu hawa wanahitaji chakula kwa wingi. Kila wadi inapaswa kupata chakula cha wiki au zaidi wanapojipanga. Magodoro yote yalibebwa na maji. Watu wamebakia bila makazi. Hata shule ambazo wao hukimbilia zimekumbwa na maji na kuta zote kuanguka. Tunahitaji msaada wa Serikali kwa dharura, na sio tu kwa kuwapatia waathiriwa kilo mbili mbili. Ni masikitiko makubwa sana kila wananchi wanapohitaji Serikali kuwasaidia inawacheza shere. Katika Kaunti ya Mombasa, Gavana alisema hajapata hata shilingi moja ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}