GET /api/v0.1/hansard/entries/1354583/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354583,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354583/?format=api",
    "text_counter": 409,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "kukabiliana na El Nino . Hatujui anayesema ukweli ni nani. Serikali kuu imesema kuwa imetoa pesa za kukabiliana na mafuriko lakini Gavana anasema hajapokea chochote. Labda wanamwambia atumie fedha za kaunti lakini pesa zimepangiwa na huwezi kutumia pesa zilizopangiwa na kuzitumia zisivyo. Hii itamletea taabu wakati wa audit . Tunaomba Serikali ilichukulie jambo hili kuwa muhimu sana na kulitilia maanani. Watu wanateseka sana, na haswa katika eneo Bunge la Kisauni linahitaji msaada. Tumehangaika sana. Maji yanafika hadi magotini. Sisi huko ni maskini sana. Vyoo vyetu vingi huwa ndani ya nyumba. Kwa hivyo, maji yakijaa vyooni yanaingia vyumbani. Hali hii ni hatari sana. Kuna uwezekano wa mkurupuko wa maradhi. Tunataka Serikali kulenga eneo Bunge hili kwa kuleta dawa katika hospitali na iruhusu watu kutibiwa bure kwa sababu ya hali hii. Shule nyingi zimetumbukia majini na tunaomba misaada kutoka mashirika mbalimbali. Hata sehemu ya Mandera South, nimeona mifugo wakisombwa na maji. Wao pia wanahitaji msaada. Isiwe tu tunazungumza hapa bali Serikali itilie maanani jambo hili kwa kuwa wananchi wanapata taabu. Hali ya uchumi ni mbaya. Bei za vyakula ziko juu, hakuna mtu anaenda kazini na watoto ni wagonjwa. Tunaomba msaada kutoka kwa Serikali. Ni haki ya wananchi kusaidiwa wakati dhiki inapoingia. Kisauni tumeumia zaidi. Tunaomba Serikali itilie maanani maneno haya na kujua jinsi ya kusaidia wananchi wake. Ahsante sana."
}