GET /api/v0.1/hansard/entries/1354608/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354608,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354608/?format=api",
    "text_counter": 434,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Rabai, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenga Mupe",
    "speaker": null,
    "content": "nyumba za wakaazi wengi wa Rabai zimeanguka kwa sababu ya mvua nyingi. Mvua imenyesha mfululizo kwa zaidi ya siku nne. Hata chakula chote walichovuna kutoka mashambani hivi majuzi kilitekwa na mvua pamoja na maji. Ninapoongea, wakaazi wa Rabai hawana chakula. Ndio maana ninauliza Serikali ibuni mbinu itakayohakikisha wote ambao wameathirika wamepewa ufadhili wa kutosha ili wasaidike katika kipindi hiki. Katika eneobunge la Rabai, kuna wodi nne. Tuko na Mwawesa, Ruruma, Kambe-Ribe na Kisurutuni. Barabara zote zilizorekebishwa hivi majuzi na Kenya Rural Roads Authority (KeRRA) zimeoshwa na mafuriko. Pia, kuna madaraja kama yale ya Jimba, Chitswa cha Mkamba, na daraja la Ngwenzeni, ambayo yamefagiliwa na mvua hii ya El Nino kiasi cha kwamba wananchi kutoka Rabai wanapata shida kubwa saa hii. Hawawezi kutembelea maeneo mengine kwa sababu daraja zote zimesafishwa na mvua ya El Nino . Tuko na mto mkubwa unaoitwa River Kombeni unaopitia Rabai. Mto huo una maji mengi sana. Kufikia wakati huu, maji haya yanaenda Bahari Hindi. Nimesimama hapa kama Mbunge wa Rabai na ningependa kusema kwamba Eneobunge la Rabai limekuwa na shida ya maji kwa zaidi ya miaka kumi. Ndio maana ninauliza Serikali ibuni mikakati katika sehemu kama hizi ambapo maji mengi yanapitia kwenda baharini. Nimeuliza serikali, ninanyenyekea. Serikali ibuni mikakati ya kujenga bwawa pale Mto Kombeni ili maji yanayopitia Mto Kombeni yatumiwe na wakaazi wa Rabai ili shida ya maji iishe. Nikimalizia, ninamshukuru Naibu wa Rais kwa kuita viongozi wote wa Kenya ili kuzungumzia swala hili la janga la mafuriko. Ninasema kwamba nina imani kuwa serikali itatoa mwongozo ili Wakenya wote ambao wamepata shida kwa sababu ya mvua ya El Nino wapate suluhu. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono."
}