GET /api/v0.1/hansard/entries/1354726/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1354726,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354726/?format=api",
"text_counter": 80,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nime bonyeza nikiwa na hakika kwamba nitazungumzia Mswada huu kuhusu kuzuia wizi wa mifugo ambao umeletwa na Sen. Cherarkey. Mswada huu unafaa zaidi wakati huu. Sehemu nyingi nchini Kenya, hasa Bonde la Ufa, wananchi hupatwa na shida za wizi wa mifugo. Wizi wa mifugo ni jambo ambalo limesumbua watu wetu kwa miaka mingi. Wakaazi wengi wa Kaunti ya Laikipia hutegemea kilimo cha mifugo kuwapeleka watoto wao shule. Mifugo ndio tegemeo lao kubwa la maisha. Kilimo cha mifugo ndio chanzo cha kuuana kwa waakazi wa kaunti yetu. Watu wengi katika maeneo ya Wangwashe, Ol Moran na Mateku, wamepoteza maisha yao kwa sababu ya wizi wa mifugo. Wizi huu wa mifugo sio wa kawaida. Hapo zamani, watu walikuwa wanashambuliwa na mifugo yao kuchukuliwa. Wakati huu, wanashambulia na kuua watu."
}