GET /api/v0.1/hansard/entries/1354728/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354728,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354728/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Baada ya kuua watu, mifugo hupelekwa mahali fulani kufugwa na kisha husafirishwa hadi miji mikuu nchini. Sio wizi wa kawaida ambao hufanywa na walala hoi. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu ya kipengee ambacho kinasema wezi wa mifugo wakipatikana, watachukuliwa hatua dhabiti za kisheria. Siyo wezi wa mifugo peke yao ambao watachukuliwa hatua za kisheria pia wafanyibiashara ambao huhusika na wizi huu. Hii ni kwa sababu wao ndio wanawafanya vijana wetu kuasi shule na kujihusishe na wizi wa mifugo. Kwa hivyo, sio wahusika wadogo ambao huiba mifugo wanaopaswa kuchukuliwa hatua pekee yao, bali watu wote wanaojihusisha biashara hii ya wizi na uzaji wa mifugo hiyo. Biashara ya wizi wa mifugo ikisimamishwa, hata wezi rejareja wanaofungulia mifugo ya watu wengine watakoma. Mswada huu ukipita, wizi wa mifugo utakuwa jambo la sahau katika Kaunti ya Laikipia na sehemu zingine nchini. Najua maendeleo mengi yataweza kupatikana. Naunga mkono Mswada huu na ninaomba tuupitishe haraka iwezekanavyo."
}