GET /api/v0.1/hansard/entries/1354822/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354822,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354822/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niyachangie mawazo yangu kuhusu sheria hii ambayo Sen. Cherarkey anataka kuleta hapa Bungeni. Mambo mengi yamesemwa lakini sitayarejelea. Kuna jambo moja ningependa kusema kwa ufupi; shida kubwa ya wizi wa mifugo ambayo tumekuwa tuking’ang’ana nayo tangu tupate uhuru. Kama alivyosema Sen. Cheptumo, ni utamaduni mbaya. Kuna tamaduni nzuri na kuna tamaduni mbaya za Kiafrika. Sheria hii ambayo Sen. Cherarkey ameleta inaongea kuhusu mambo mengi na mazuri. Lakini kuna kitu kimoja ambacho ningependa Sen. Cherarkey akifikirie na pengine aiongeze kwenye mawazo ambayo ameandika kutoka kwa waheshimiwa walioongea."
}