GET /api/v0.1/hansard/entries/1354826/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1354826,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1354826/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "na kuelezwa kuwa utamaduni huu haufai kwenye miaka ya kisasa. Mbali na mambo yaliyopendekezwa lazima tugeuze akili ya wananchi. Tusipofanya hivi, tutawafunga vijana wangapi? Badala waende shule tutakuwa tunawafunga. Pili, wananchi waelezwe sheria itakayopendekeza kiwango cha ng’ombe na mbuzi kitakacholipa mahari; katika sehemu fulani mahari isipite ng’ombe tatu ama kuku wanne. Watoto wetu waoane kihuru. Watu wasiibe ng’ombe kwa sababu wanataka kuoa. Sheria hii lazima iangalie shida hii. Kuna tamaduni mbaya ambazo hatuwezi maliza na sheria pekee, lazima tuelimishe watu, tuwabadilishe akili zao na kuweka mifano ya vile tamaduni zitafuatwa. Kwenye Kaunti lazima kuwe na makubaliano kwamba mzee akiitisha ng’ombe 100 ama mbuzi 50 akamatwe. Watu waelewe kuwa kuweka mahari ya juu inasababisha wizi wa ng’ombe na mbuzi. Hizi ndizo shida ambazo tunajaribu kutatua. Ikifika miaka ya ndoa, tuwache wasichana waolewe. Ukikaa na wao wataibiwa ama kuzalishwa. Tusiweke mahari ya juu. Kwa kila kaunti mahari iwe kidogo ya kutosha ili vijana wasipate moyo wa kuiba. Ikiwa nataka kuoa na yule msichana ananiambia lazima nitoe ng’ombe 300. Kule South Sudan mahari ni takrimu ng’ombe 300. Nikimpenda msichana, hata kama kuna hii sheria ya Sen. Cherarkey, nitaiba ng’ombe. Sen. Cherarkey, kwenye hii sheria, weka taratibu za kulipa mahari ili tusipate shida ya vijana wetu kufungwa kwa ajili ya mambo kama haya. Sheria hii ikarabatiwe ili kuelimisha watu wetu watoke kwa tabia potovu na waingie kwenye miaka ambayo tunaishi. Asante, Bi. Spika wa Muda. Naunga mkono."
}