GET /api/v0.1/hansard/entries/1356485/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356485,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356485/?format=api",
"text_counter": 304,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kenya ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Kamati ya Usalama ya Umoja wa Mataifa waliketi na kusema ya kwamba wale ambao wana ujuzi, uzoefu na uwezo wa kuongoza katika nchi ya Haiti ni Kenya. Nimewasikia ndugu zangu kutoka upande wa upinzani wakisema ya kwamba tunapaswa kuzipinga juhudi hizi. Tunapaswa kupongeza askari polisi wa nchi ya Kenya kwa kuteuliwa ili kuongoza kwa sababu wana uzoefu na ujuzi. Kabla ya kupitisha Hoja hii, nimekuwa nikipigiwa simu na askari polisi ambao wana uzoefu wakisema kuwa wanangoja tuipitishe Hoja hii ili Wizara ya Maswala ya Mambo ya Ndani iweze kuwapeleka kule kufanya hii kazi ambayo wanaijua Zaidi. Hawa polisi wanapiga simu kwa sababu wamewaona ndugu zetu askari ambao wameenda katika---"
}