GET /api/v0.1/hansard/entries/1356497/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1356497,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356497/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kifungu cha 108, police service ni polisi ambao wanatulinda katika nchi ya Kenya. Polisi hawana majukumu ya kufanya ulinzi katika nchi za kigeni isipokuwa mahali ambapo kuna reciprocation, yaani tunawapa polisi wetu na wale pia wanatupa polisi wao kuja kujifunza kazi katika nchi yetu. Wakati huu nchi yetu haina polisi wa kutosha. Inasikitisha kwa sababu watu wanaendelea kuuawa katika sehemu mbali mbali nchini Kenya. Katika Kaunti ya Baringo na sehemu za Turkana, watu wanauliwa kiholela. Sehemu nyingi katika nchi yetu zina utovu wa usalama. Ni makosa kwamba sisi wenyewe hatuna polisi wa kutosha na tunawapeleka wale wachache tulio nao katika nchi nyingine kuhudumu kwa muda usiotambulika kulingana na ripoti tunayoijadili hapa Bungeni. Sisi kama Kenya hatuna askari wa kutosha. Katika Kaunti ya Mombasa benki zingine zinalindwa na askari wa jela. Polisi wa jela wanasaidia ulinzi katika mji wa Mombasa. Polisi wetu ni wachache. Haiwezekani kuwa wale polisi wachache ndio wanatumwa kwenda nchi nyingine."
}