GET /api/v0.1/hansard/entries/1356522/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1356522,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356522/?format=api",
    "text_counter": 341,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, naunga mkono polisi waende kuhifadhi usalama kule Haiti. Hawa ni watu wenye ujuzi wa kutosha na Mungu atawapa baraka. Namkumbusha Sen. Oketch Gicheru kwamba tulipigana vita na mzungu bila mafunzo yoyote na tukashinda. Kwa hivyo, hawa vijana wetu wakienda Haiti watashinda kwa sababu hivi sio vita vya kufikiria. Ni vita vya dhidi ya ndugu na dada yake. Ni kwenda na wale ambao wamesoma ili wakalishe vikundi tofauti pamoja na kuleta masikizano. Waambiwe dunia hii inaisha kwa sababu tunataka tuondoke. Tunaposoma Bibilia, tunaona akina mama wawilli walikuwa wanapigania mtoto. Watu walikuwa wanawapita bila kuwasaidia. Hata hivyo, kukaja mtu mmoja ambaye alitumia ujuzi na kuuliza kila mama angetaka mtoto afanyiwe nini. Mama mmoja akasema kwamba angetaka mtoto apasuliwe mara mbili ili kila mama apate nusu ya mtoto. Mama mwingine alisema kwamba mtoto apewe yule mama mwingine na vita vikaisha. Kwa hivyo, naomba hawa vijana wetu waende Haiti. Tunafaa tujivunie kwa sababu ilisemekana Kenya iko imara na inaelewa mambo ya usalama. Tumeulizwa tusaidia nchi ya Haiti ili ipate usalama. Jambo la mwisho ni kwamba, tuwasaidie ili waweze kwenda na warudi salama. Kama mashujaa wanaomjua Mungu inafaa tuwaombee ili waende na warudi na taarifa nzuri ya kuwa hiyo nchi imesimama imara. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono."
}