GET /api/v0.1/hansard/entries/1356612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356612,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356612/?format=api",
"text_counter": 431,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Kahawa ndio bidhaa ya pili yenye mauzo ya juu duniani. Mafuta ndiyo ya kwanza. Kwa muda mrefu sana, wakulima hawa wamekuwa na shida nyingi kwa sababu ya wakiritimba ambao hufaidika kutoka kwa mazao ya kahawa. Mkulima anapopeleka kahawa katika kiwanda cha kusagia, mambo yake yanafika pale. Kahawa inapelekwa kwa millers, agents, marketers na brokers kabla kufika soko kuu la kahawa, Nairobi Coffee Exchange (NCE). Mkulima hatajua bei ambayo anafaa kuuza kahawa yake. Kahawa, majani chai na bidhaa zingine, ndio baadhi ya mazao yanayopelekwa sokoni na wakulima wasijue bei. Bei ya kahawa imekuwa inatolewa na wanunuzi. Wakulima hawajaweza kupata bei nzuri ambayo inaweza kusimamia ukuuzaji wa kahawa na kugharamia pembejeo na vitu vinginezo ambavyo vinatumika. Bw. Spika wa Muda, kabla sijaudhamini Mswada huu, nilikuwa nimetembea katika nchi ya Amerika na nikapata wanauza kahawa iliyotoka kiwanda kimoja cha Kaunti ya Kirinyaga - Rungéto. Robo ya kahawa hiyo ilikuwa takriban USD8. Hesabu niliyofanywa wakati huo, kusema ukweli, kilo moja ya kahawa ile ilikuwa inanunuliwa zaidi ya Kshs9,800. Wakulima wa Rungéto mwaka huo walilipwa Kshs100 kwa kilo moja. Pesa ambayo mkulima alilipwa kulinganishwa na pesa ambayo kahawa ilinunuliwa, inaonyesha kuwa wakulima wa Kenya wamenyanyaswa sana. Wakulima wanafanya kazi ngumu ambayo inaitwa na Waswahili kazi ya msaragambo. Baada ya kufanya hii kazi hawafaidiki. Kahawa ni mojawapo ya bidhaa ambazo zinauzwa kupitia vyama vya ushirika. Kuna mpangilio maalum ambao unatumika katika ukuzi na uuzaji wa kahawa. Millers ambao wanasiaga kahawa, bado wanajiita agents, wanasimamia kuuza kahawa na pia ni"
}