GET /api/v0.1/hansard/entries/1356616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356616,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356616/?format=api",
"text_counter": 435,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Pesa zitakazokusanywa zitafikia mkulima ili kuondoa wakiritimba ambao wanapangia pesa ya mkulima pasipo kumhusisha. Jambo la pili ni Warehouse Receipt System. Usimamizi wa kahawa katika maghala baada ya kuchunwa na kuwasilishwa. Mkulima anapopata mnunuzi wa kahawa hata kama ametoka nje ya nchi, lazima kuwe na idhini na makaratasi ambayo itapigwa sahihi kuhakikisha kwamba amekubaliana na bei ya kahawa na pia amekubali kuuza kahawa yake. Mswada huu umependekeza njia mbili za kuuza kahawa. Mkulima anawezawasilisha kahawa katika soko la kahawa la Nairobi Coffee Exchange. Pia anaweza kuuza kahawa moja kwa moja hadi nchi za ngámbo. Kwenye njia hizi mbili, pesa itapitia kwenye DSS. Nilibahatika kutembelea nchi ya Colombia wakati tulikuwa tukirasimu Mswada huu. Tuliona mafanikio iliyo kwenye nchi ile wakati uuzaji na uzalishaji wa kahawa unazingatiwa. Nchi ya Colombia ina extension officers. Mji wa Pereira una researchers. Mswada tuliowasilisha unapendekeza kubuniwa kwa Coffee Research Institute (CRI). Colombia ina watu zaidi ya mia moja ambao wako na uzamivu kwenye sekta hii. Nchi hii"
}