GET /api/v0.1/hansard/entries/1356626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356626,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356626/?format=api",
"text_counter": 445,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "na brokers . Zaidi ni kwamba walikuwa hata wanaenda nchi za ng’ambo, wanasajili kampuni na kuja kama wanunuzi. Kwa mafano, kahawa ya Kibirigwi ikiletwa, walikuwa wanakaa pamoja na kusema watanunua hiyo kahawa tena bei fulani. Ina maana kwamba walikuwa wanajua watanunua kahawa kwa bei gani. Kwa hivyo, inakuwa vigumu sana mkulima wa kahawa kufaidika kwa sababu wanunuzi wa kahawa walikuwa wananyanyasa wakulima. Ndio maana tuliona ni vizuri kuwe na sheria nzuri ambayo inalinda wakulima wa kahawa ili wafaidike baada ya kazi ngumu. Bw. Spika wa Muda, nadhani wengi wetu hapa tunakunywa kahawa. Jambo la kushangaza ni kwamba, kahawa yoyote ambayo unaweka kwa kikombe, unakoroga na inayeyuka yote, kwa kimombo inaitwa instant coffee, hiyo sio kahawa ya Kenya. Hiyo ni Robusta coffee ambayo inatoka kwa majirani. Hii ni kusema kamba sisi Wakenya hatutumii kahawa yetu. Kwa hivyo, katika Mswada, tumesema tuwe na kodi asilimia 200 ambayo itakuwa inakatwa kwa kahawa yoyote ambayo inatoka nje kuja kutumika humu nchini. Katika hiyo asilimia 200, asilimia 100, itapelekwa kwa Coffee Research Institute (CRI), itumike katika kuboresha utafiti wa kahawa. Asilimia 0.5 itaenda kwa serikali za kaunti ambazo zinalima kahawa. Hii ni kwa ajili ya miundomisingi na barabara zinazotumika. Asilima 0.5 itaenda kwa Coffee Board of Kenya (CBK). Bw. Spika wa Muda, huu Mswada uko na mambo mengi mazuri. Wakati ripoti itakuwa hapa, Maseneta wataingalia. Kwa hivyo, naomba Maseneta wasome na waunge mkono hiyo ripoti ya kahawa. Tukifanya hivi, tutahakikisha ya kwamba wakulima wa kahawa wanasaidika katika kaunti zote ambazo zinakuza kahawa. Kaunti zinazokuza kahawa humu nchini ni nyingi ."
}