GET /api/v0.1/hansard/entries/1356628/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356628,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356628/?format=api",
"text_counter": 447,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Katika Kamati yetu ya Ukulima, Ufugaji na Uchumi Samawati, tumeangalia Miswada kadhaa inayohusisha kila kaunti katika nchi hii. Mojawapo ni marekebisho ya sheria ya AFA 53 ya 2013. Hii sheria inasema makadamia, bixa na korosho zinafaa kuuzwa zikiwa zimetolewa maganda. Hili jambo limekandamiza wakulima sana. Kwa hivyo, tumeshughulikia kila eneo. Sasa tuko na sheria inayohakikisha kuna zao ambalo linapatia wakulima pesa katika kila eneo. Tuko na Mswada wa pamba ulioletwa na Mwanakamati wangu, Sen. Beth Syengo. Kuna Mswada wa mchele, 2023 ambao nimeleta mimi. Tuko na Mswada wa kahawa, korosho na huu wa kushughulikia ufugaji. Kwa hivyo, ninaeomba Maseneta wote waunge mkono Mswada huu ili tushirikiane katika kuokoa wakulima katika nchi hii. Ninamwomba Seneta wa Kaunti ya Kiambu, Sen. Thang’wa, aunge mkono Mswada huu. Asante."
}