GET /api/v0.1/hansard/entries/1356913/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356913,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356913/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Garsen, ODM",
"speaker_title": "Hon. Ali Wario",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa fursa hii. Ningependa kumpongeza Rais kwa Hotuba nzuri. Ninakata kuongea kuhusu usalama wa nchi. Inashangaza sana wakati Serikali inatia bidii ili usalama upatikane katika nchi yetu ya Kenya, jamii zinazidi kuzozana. Inafaa tutafute kiini kinachosababisha jamii kukosana. Labda Serikali haitumii mbinu mwafaka, ya kusaidia jamii kuishi kwa amani. Kwa hivyo, ninasisitiza jamii kwanza. Wazee, ambao ni kitengo muhimu sana, pamoja na viongozi wahusishwe katika mambo ya usalama. Haiwezekani mtu katika ofisi ya Serikali kuamini kwamba kuleta usalama ni kutumia nguvu, mabavu ama unyanyasaji. Hivyo, hatuwezi kusaidika. Ninampongeza Rais kwa hiyo Hotuba kuhusu mambo ya usalama. Kwamba jamii ihusishwe na hasa wazee na viongozi. Ni ajabu sana kwamba waziri anaweza kuzuru sehemu fulani kuangalia usalama bila viongozi waliochaguliwa kuhusishwa. Hiyo haiwezekani. Ndiyo maana amani haipatikani katika sehemu za Rift Valley . Hata serikali ikipeleka jeshi kule, hawawezi wakaleta usalama. Jambo lingine kuhusu usalama ni kwamba vijana wanapotezwa kwa kusingiziwa mambo ya ugaidi; labda na viongozi wa dini... Lazima serikali ibadilishe mbini na kujua vijana wanaoshukiwa kuwa wagaidi. Ni nini inasababisha ugaidi? Labda hawahusiki na wanasingiziwa tu ama ni mambo ya food insecurity na njaa. Lazima haya mambo yaangaliwe. Jambo lingine ni kuhusu subsidised fertiliser . Wengine wetu ni wafugaji. Serikali inasisitiza kuhusu ukulima wa kahawa, majani chai, mahindi na kadhalika. Huwezi kula ugali bila mboga na nyama. Kwa hivyo, Serikali iangazie ufugaji na iweke pesa sawa sawa ili ufugaji uendelee. Hii ni kwa sababu, ufugaji unahusiana na culture na kuchangia pakubwa katika uchumi wa nchi yetu. Ufugaji lazima uangaliwe. Wakulima wamelima na mafuriko yana waathiri pakubwa kwa sababu mimea imetoa mazao na sasa inabebwa na maji. Kwa hivyo, ninaomba Serikali ifikirie mbinu za kupatia fidia kwa jamii zilizoathirika ili watu wawe na moyo wa kulima zaidi. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuwasaidia kutokana na dharura ya mafuriko. Kuhusu Housing Programme, inafaa waanze na watu walio kule mashambani kwa sababu wanahama kutoka huko kuja town . Lakini, wakijengewa kule mashambani, watabaki huko wawekewe maji, wapewe usalama, barabara na kadhalika ili wawe encouraged kuishi huko. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}