GET /api/v0.1/hansard/entries/1356922/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356922,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356922/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii nichangie Hotuba ya Rais wetu. Alikuwa Bungeni na akatueleza mambo mengi ambayo amepangia nchi yetu ya Kenya. Ninachukua nafasi hii kumpongeza. Tunapozungumzia maendeleo nchini, sisi sote tunaelewa jinsi mambo yalivyokuwa Rais aliposhika hatamu ya uongozi. Tunaelewa kulikuwa na changamoto katika uchumi wa nchi hii. Rais angechukua mkondo wa kuomba madeni kutoka nchi zingine, angependwa sana na watu wengi. Lakini kama kiongozi anayewajibika kwa wananchi wa Kenya, ameamua kushughulikia mambo ya Wakenya. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza kwa kukataa kuchukua madeni. Madeni sugu nchini yalichukuliwa bila ya Wakenya kujua. Nainmpongeza kwa kufika Bungeni na kutoa taarifa yake. Mambo ya affordable housing yameanzishwa na yanaendelea. Ningependa kumjibu Mbunge wa Bondo aliyesema kuwa Rais wetu huongea mambo mengi bila utekelezi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}