GET /api/v0.1/hansard/entries/1356923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356923,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356923/?format=api",
"text_counter": 283,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": "Ninashangaa sana kwa nini Mbunge mzima anaweza kusema kuwa Rais husema mambo mengi bila kutekeleza. Ametekeleza mambo ya affordable housing na subsidized fertilizer. Wananchi wa Kenya wamechukua mbolea, wamelima na wana chakula kingi hivyo kutatua shida ya njaa katika nchi yetu. Nilifurahia sana aliposema anataka kuaibisha njaa katika nchi yetu ya Kenya na kusema ukweli amefanya hivyo kwa sababu ametupea mbolea ya bei nafuu. Kama Mbunge, mimi pia ni mkulima, na nimefurahia hiyo fertilizer kwa sababu imeniwezesha niwe na mavuno ambayo yamenisaidia kwangu kwa mambo ya chakula. Sitaenda tena madukani kununua vyakula. Watu wengi pia walipata mavuno mengi na hata wakauza mengine."
}