GET /api/v0.1/hansard/entries/1356924/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1356924,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356924/?format=api",
    "text_counter": 284,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": "Jambo lingine ni lile la Hustler Fund ; akina mama na vikundi vyao ndio wamechukua pesa hizi kwa wingi. Hizi ni pesa ambazo zimehesabika kwa mabilioni na ninafurahi sana kwa sababu watu wamefaidika. Hakuna mtu ambaye amekaa tu kiholela nyumbani kwa sababu ya kukosa pesa. Ni ukweli kwamba tuko na ugumu kidogo katika mambo ya uchumi katika nchi yetu ya Kenya, lakini hatuwezi tu kuketi na kulia. Tumesikia mambo ya Rais wetu. Wananchi wachukue fertilizer na loan ndio waendeleze biashara zao. Ningependa pia kugusia jambo la ommunity health promoters, watendakazi wa serikali ambao watakuwa wakilipwa na County Government na serikali kuu kutembea nyumbani kuangalia afya za wananchi ili waweze kutatua shida za wagonjwa mapema. Mtu akionekana mapema kwamba ana tatizo fulani, anaweza kutibiwa kwa wakati unaofaa. Haya ni mambo ya kutatua matatizo ya afya katika nchi yetu. Afya, chakula na uendelezaji biashara ni mambo ya maana sana. Ningependa kumpongeza Rais wetu kwa kuzingatia climate change . Jumatatu tulifanya upanzi wa miti katika nchi yetu. Ninaamini tulipanda miti zaidi ya billioni moja. Hiyo ni hatua maalum ya kuhakikisha kuwa tunatatua mambo ya climate change na mazingira nchini. Ninampongeza sana kwa kusema heko. Mungu akusaidie. Tuko nyuma yako. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}