GET /api/v0.1/hansard/entries/1356931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1356931,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356931/?format=api",
"text_counter": 291,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa ya kuchangia Hotuba hii ya Mhe. Rais iliyokuwa hapa Alhamisi iliyopita. Kwa kweli, Wakenya wengi walitegemea kusikia ni vipi hali ya gharama ya maisha itashuka ama kupunguzwa makali yake. La kusikitisha ni mizigo mizito ya kodi kwa Wakenya. Hatupingi kodi lakini mapato ya Wakenya yanazidi kupungua. Hivi sasa watu wananunua unga robo. Tujiulize sisi hapa: Ni vipi tutakunja sera ya kodi bila kuvunja migongo ya Wakenya? Mhe. Spika wa Muda, Kenya si Ulaya wala Marekani. Sera ya kodi yafaa kuzingatia hali ya uchumi. Ifahamike kwamba uchumi wetu hutegemea wengi ambao mapato yao ni ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}