GET /api/v0.1/hansard/entries/1356933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1356933,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356933/?format=api",
    "text_counter": 293,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, anapofika shambani, lile tingatinga linalolima linatumia mafuta ambayo ni gharama vile vile. Akimaliza, mazao yanakuwa ni mengi kweli. Lakini, kuyasafirisha mpaka viwandani anatumia tena vyombo vya mafuta. Akifika viwandani vile vile, kama ile bidhaa ni ya kusagwa, inatumia mafuta tena kusaga ambayo bado ni gharama. Akitoka pale kupeleka sokoni, bado anatumia gharama tena kubwa zaidi. Cha muhimu ni tuangalie vipi tutashukisha bei ya mafuta kwa sababu ndiyo inachangia kila jambo ambalo linafanya hali ya maisha kuwa magumu. Mbolea ni sawa lakini bei ya mafuta lazima iangaliwe vipi itashukishwa. Watu wengi, hasa wa Kisauni na pwani kwa jumla, wanataka kunufaika kutokana na rasilimali zilizo katika sehemu zetu kama bahari, mbuga za wanyama pori na madini. Katika Hotuba ya Rais, hakuna chochote kilionyesha vipi tutafaidika na rasilimali zetu."
}