GET /api/v0.1/hansard/entries/1356934/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1356934,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1356934/?format=api",
    "text_counter": 294,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Suala la kulaumu Serikali iliyopita lazima likome na liishe kwa sababu tangu Serikali hii ichukue mamlaka ni mwaka mzima. Vipi tunakaa na kulaumu ile Serikali iliyotoka? Hata watu wamewasahau waliotoka. Vipi nyinyi mko hapa bado na mnawalaumu? Kaeni chini muone mna mipango gani ya kuweza kuboresha hali ya maisha badala ya kulaumu Serikali iliyopita. Kuhusu ajira ya walimu 56,000, kwa kweli inatangazwa tu lakini wengi hatuoni. Kama ingefanywa kihaki, kila eneo bunge lingepata walimu 193. Angalau, kila mtu angeona walimu wameajiriwa. Ukija katika Eneo Bunge la Kisauni, ni walimu wawili pekee ambao wameajiriwa. Hatuhisi kama walimu wameajiriwa. Lazima kuwe na usawa. Ikiwa ni ajira kwa Wakenya, ni ajira ya Kenya nzima. Hata kama tunataka kukamua ng’ombe, tumbakishie ndama wake pia apate. Tusimkamue ng’ombe mpaka atoe matone ya damu. Wakenya wengi hawakutegemea yale ambayo yalizungumzwa. Walitegemea mengi ambayo yangewanufaisha. Wananchi wanaumia. Hali ya uchumi ni mbaya. Hakuna fedha mifukoni. Mtoze kodi mtu aliye na pato. Kwa hayo, Mhe. Spika wa Muda, wacha nipatie wengine fursa pia wachangie. Asante sana."
}