GET /api/v0.1/hansard/entries/1357434/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1357434,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1357434/?format=api",
    "text_counter": 460,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "elimu bora na ya nafuu. Hayo ni maswala ambayo Rais angefaa ayaongelee na tuone kwamba amepeana suluhisho la kudumu kwa wazazi ili kupambana na elimu ya juu. Bw. Spika wa Muda, jambo lingine ni bei ya petroli na mafuta. Ameacha pengo kubwa sana kwa kukosa kuguzia petroli na mafuta. Hii ni kwa sababu kupanda kwa bei ya petroli na mafuta inaleta ongezeko kubwa sana kwa bei ya usafiri na chakula, hususan chakula ambacho kinatoka kwa viwanda. Kilimo cha umwagililaji wa maji pia kinatumia mafuta na hii inafanya bei kuongezeka. Tegemeo kubwa la mashini ya kilimo inategemea petroli. Hiyo pia ni changamoto. Nikimalizia, tumeona kwamba Rais hakuwa na ramani ya kina ya kuleta mabadiliko ya uchumi. Vile vile, hakuleta mikakati wala hatua zozote ambazo zitaweza kuchukuliwa kubadilisha uchumi wetu. Kwa hivyo, tunaona kwa jumla kwamba kuna maswala nyeti ambayo hakuyaguzia. Hayo ni maswala ya mafuta, elimu, kupanda kwa bei ya maisha na maswala ya kina ya ramani ya kubadilisha uchumi. Tunajiona kwamba bado tuko pale pale, tunahangaika na maisha. Hatukupewa suluhisho lolote la kudumu la kubadilisha maisha ya mkenya, kupunguza bei ya maisha na elimu ambayo ni kigezo kikubwa sana. Watoto wanakaa manyumbani, hawasomi. Elimu inabadilika hivi na vile, gharama ya kila aina kwa mzazi ambayo imekuwa ngumu. Kwa hivyo, tunaomba Rais aangazie hayo maswala muhimu ambayo yanamfinya mwananchi wa kawaida. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}