GET /api/v0.1/hansard/entries/1357436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1357436,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1357436/?format=api",
    "text_counter": 462,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Naunga mkono Rais wa Kenya kwa ile Hotuba yake ya siku ya Alhamisi. Ingawaje kuna wajumbe ambao hawakuhudhuria kikao hicho, mazungumzo yake yalikuwa mazuri kwa sababu yaliguzia mambo ya deni. Kaunti zimekuwa na madeni mingi na zimepewa pesa za kulipa deni hizo. Na pia, alipata Kenya ikiwa na madeni mengi kutoka kwa serikali iliyopita lakini anaendelea kuyalipa. Jambo lingine aliloligusia ni swala la kilimo. Hakusema ni kaunti gani za kilimo. Katika Kenya, tuko na kaunti 47 na hakusema ni Busia ama Embu. Alisema amepunguza bei ya mbolea kutoka Kshs6,500 hadi Kshs2,500 ili kila mtu apate chakula kwa sababu kila mtu amekubali kulima. Wale watu ambao wanadanganya wengine ili wavae sufuria kwa kichwa wawache. Pia, alizungumza kuhusu elimu. Kwa elimu, walimu hawajaajiriwa kwa kipindi cha miaka 10. Watu wengi wamesomea elimu na wakawacha kutaka kuwa walimu. Lakini kwa sasa, ameajiri walimu 50,000. Pia, aliguzia mambo ya afya. Wafanyakazi wengi wa afya walikuwa wanafanya kazi bila kulipwa. Ametoa hayo mambo yote kutoka kwa Serikali kuu akapeleka kwa serikali gatuzi na hata mashinani. Jambo lingine ambalo alizungumzia ni jambo la nyumba. Wale watu ambao hawajiwezi watukuwa na nyumba kwa kipindi kifupi kijacho. Jambo lingine alilolizungumzia ni kupanda miti kutoka Serikali ya juu hadi vijijini. Tulishuhudia aliposema kwamba siku ya Jumatatu iliyopita, iwe likizo ili kila gavana katika kaunti zetu"
}