GET /api/v0.1/hansard/entries/1357438/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1357438,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1357438/?format=api",
    "text_counter": 464,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "apande miti. Hadi alitoa asilimia tano ya pesa za National Government Constituency Development Fund (NG-CDF) ili zitumike katika shughuli ya kupanda miti. Alisema mambo mengi. Pia akasema kuwa kila kaunti ijengewe Industrial Park ili watu wawe akipeleka mavuno yao ili kukuza biashara na mambo yawe mazuri. Nikimalizia, Rais aligusia hata mambo ya disability. Kuna kisa kilichosimuliwa ambapo watu wawili walijenga nyumba. Mmoja alijenga juu ya mwamba na mwingine juu ya mchanga. Wakati mvua ilinyesha, nyumba iliyojengwa juu ya mchanga ilibomoka na kuanguka kwa sababu ya uzito. Kwa upande mwingine, nyumba iliyojengwa juu ya mwamba, ilisimama. Wakenya, tuko kwa shida lakini nina wahakikishia kuwa Serikali ya Kenya Kwanza tunajenga nyumba juu ya mwamba. Tunajua kuwa tutashinda vita hivi vyote. Kwa hivyo, ninaomba tuungane Maseneta wote na tuunge mkono Serikali ya Kenya Kwanza."
}