GET /api/v0.1/hansard/entries/1357546/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1357546,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1357546/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi. Swali langu ni fupi. Kule kwetu Tana River tuko na shida kubwa sana ya wanyama. Kwanza nataka Waziri aifanye priority. Afanye safari tupange akuje awasikize wananchi vile Tana River tunaumia. Watu wanakufa sana. Lakini, swali langu ni hili: Ni mipango gani ambayo Waziri ako nayo kuongeza askari wa Kenya Wildlife Service (KWS)? Mara nyingi hawa ndio huwa wanatusaidia, lakini ukiangalia, wamepunguzwa kabisa. Ukiangalia sehemu ya Delta, hapa kati kati Tana River Sub County, ukiangalia Tana North Sub County, wamepungua badala ya kuongezeka na shida zetu zinazidi kuongezeka. Je, Waziri, ni mipango gani ambayo uko nayo kutuongezea wasimamizi wa wanyama wa pori katika gatuzi ndogo la Tana River? Asante."
}