GET /api/v0.1/hansard/entries/1357619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1357619,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1357619/?format=api",
"text_counter": 168,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Nimeangalia shughuli ambazo wamekuwa wakiziangatia. Wamekutana na Wizara ya Afya, Wizara inayohusika na Mambo ya Maswala ya Nje, na Wizara inayohusika na Mambo za Humu Nchini. Lakini, ni vizuri tuseme ya kwamba, muda huu ambao wameuliza wautumie vizuri wasije tena hapa kuomba waongezewe. Hii ni kwa sababu mambo waliyoyafanya, wameyafanya na zaidi ya siku 165. Haya ni mambo machache yaliyobaki wanayotakia siku 100, najua inawezekana. Hii ni kwa sababu wanasema wanataka kukutana na Mkuu wa Sheria, Balozi wa nchi ya Marekani na vile vile, watembelee nchi ya Amerika ndio waweze kukutana na Seneti ya Amerika. Kwa hivyo, hizo siku 100 zitatosha ili waweze kushughulikia Wakenya ambao waliathiriwa na vile, wale ambao tayari waliaga, wale watu wao ambapo ni zaidi ya 200, wapate fidia. Naipongeza hii kamati kwa kazi nzuri wanayofanya lakini wasiongeze siku kupita hizo siku 100 ambazo wameitisha. Hii ni kwa sababu ni mambo machache sana yaliyobaki na hatutakataa kwa sababu tayari wamemkula ng’ombe, iliyobaki ni mkia. Hizo siku 100, waweze kumaliza mkia, walete ripoti na Wakenya wetu waweze kushughulikiwa."
}