GET /api/v0.1/hansard/entries/1357846/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1357846,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1357846/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Mhe. Spika, ninakuomba utembeze Wabunge, hasa Lamu East. Mwalimu anayefunza Lamu East ananunua maji lita ishirini kwa Ksh50. Huwezi kumfananisha na mwalimu anayefunza Nairobi au kaunti nyingine. Mtu aliye Kiunga analipa Ksh8,200 ndiyo apate kitambulisho. Nilivyoona Wakenya wanalalamika kulipishwa Ksh2,000 kupata kitambulisho, nilisema ni sawa walipe kama tunavyolipa sisi. Ninaweza kufanya hesabu rahisi. Ukitoka Ishakani, pikipiki ni Ksh300 mpaka Kiunga. Kutoka Kiunga hadi Mkokoni kwa gari ni Ksh700. Kutoka Mkokoni, upande boti hadi Mokowe ulipe Ksh3,000. Kutoka huko, upande pikipiki mpaka kwa ofisi ya vitambulisho ulipe Ksh100. Hiyo hujalala au kula. Huwezi enda siku moja na urudi. Hiyo ndiyo inamaanisha hardship area . Kule kwetu Kiunga, Lamu East, kuna walimu wanapewa siku za mapumziko lakini hawaendi kwa sababu hawawezi kumudu kuenda nyumbani. Wanaokaa kule, haimanishi ni wabajuni peke yao. Kuna kila kabila na wanapata shida. Lakini, nyinyi mkiskia ni mgao au faida, kila mtu anataka kupata. Wabunge, muwe na busara. Kuna watu wanaumia hii Kenya mkikaa hapa. Ndiyo saa hii tunataka kufanya marekebisho. Kuna maeneo ambayo hayana hata inchi moja ya lami. Serikali hii ndiyo inaangalia mambo haya. Tulizindua barabara ya kwanza juzi juzi. Tukipeleka wanafunzi Lamu West au Mombasa, ilikuwa waende wakaone lami wajue ni nini. Kisha mnataka kujifananisha na sisi! Ninaomba wanaopanga maeneo ya ugumu wasijulikane. Ninaomba sana ili hawa Wabunge waweze kutuelewa. Tafadhali pangeni safari mkaende mwone marginalisation ama hardshiparea. Kuna askari wako Kiangwi ambao hawaogi. Wanaishi kama wanyama kwa sababu hawana maji. Kila mahali ukichimba, maji ni ya chumvi. Mhe. Spika, ninakuomba tafadhali, kwa hisani yako, panga Wabunge waende wakaone maeneo ya ugumu ili wajue inamaanisha nini."
}