GET /api/v0.1/hansard/entries/1358006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1358006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358006/?format=api",
"text_counter": 206,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Nikichangia Hoja kuhusu Hotuba aliyoitoa Rais hivi karibuni, ninajua kwamba hali ni ngumu sana katika Taifa letu. Lakini, ningependa kumweleza Mheshimiwa Rais kwamba wanaomshauri wanafaa wawe na uwazi na yeye. Si vizuri tukiona Wabunge hapa wakimpigia upito wakati wanajua kuna matatizo. Kiongozi mzuri ni anayependa kuambiwa hapa kuna shida na hapa uko sawa. Nimeona kweli Rais anajaribu kujibidiisha ila kuna maswala ambayo hakuzungumzia. Kiongozi mwema huzungumzia matatizo aliyo nayo na mazuri aliyofanya. Hatukuona hilo katika Hotuba ya Rais. Hotuba ya Rais pia, haikushika hali tata ya hisia za wananchi zilivyo katika Taifa hili. Wananchi wanahangaika na njaa, tax ziko juu, ushuru unapanda kila kukicha. Tumeona zingine katika vitambulisho. Bei ya chakula pia, imepanda juu. Kwa hivyo, wananchi walikua wanasubiri kusikia atashika maswala gani yanayogusa mwananchi wa kawaida; wa kule chini. Nikizingatia kuwa mafuta ama fuel imepanda juu, stima pia imekuwa katika hali tata katika nyumba za Wakenya wengi. Mhe. Rais pia, alikwepa kuzungumzia swala hili. Ninamweleza Rais kuwa, ndio anajaribu. Lakini, ninafikiri kuwa washauri wake hawamshauri vizuri. Inakuwa aibu kwa kiongozi wa Taifa kutangaza kuwa mvua ya El Niño haitokuwepo. Kisha anasema hawezi kuwa na mipango ya kukabili El Niño halafu sasa tuanze kuona mvua The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}