GET /api/v0.1/hansard/entries/1358007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1358007,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358007/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "inanyesha. Hii sio hoja ya Rais mwenyewe. Alishauriwa kwamba hii haitokuwa. Ndio maana ninasema huenda yeye ana nia nzuri kwa Wakenya lakini wanaomzingira na kumshauri hawamwelezi vizuri. Wabunge wenzangu, msiwe watu wa kupiga ngoma tu mkicheza na hamjui mziki waenda vipi. Hili ni Bunge la uwazi na ni lazima tuelezane ukweli. Tumwambie Rais amefanya vipi hapa, wapi kumepunguka na wapi ajibidiishe. Huo ndio mjadala unaofaa kuendelea katika Bunge hili. Si sawa tukiwa watu wa kusema twampongeza na kumpongeza wakati mambo si sawa kule nje. Hata yeye mwenyewe anapokaa anajua kweli kuwa hawa Wabunge wake hawampendi. Msifikiri kuwa Rais hana akili. Ana akili zake. Anajua na anaangalia. Anatamani Mbunge aliye upande wake amwelezee ukweli hata siku moja kuwa kuna shida; iko hivi hapa"
}