GET /api/v0.1/hansard/entries/1358009/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1358009,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358009/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": ". Mheshimiwa Rais, wananchi wanalia bei ya mafuta imepanda na hawana chakula. Tunaweza kufanya namna gani? Kiongozi mzuri ni yule anaangalia kama hali ni mbaya katika taifa. Asifanye mambo elfu moja kwa wakati mmoja. Achague jambo moja ambalo linaweza kugusa mwananchi na kuinua uchumi. Azingatie jambo moja na kulitenda kwa ubora zaidi kisha mengine yatafuata polepole. Lakini, Rais amezingirwa na mambo ya barabara, miundo msingi, agriculture . Sijui kama anataka kufanya mambo hamsini kwa wakati mmoja wakati ambapo uchumi hauko sawa. Mimi kama Mama Mombasa simchukii. Hapana. Ninampenda tena sana lakini nitakuwa muwazi kwake kusema kuwa hali si sawa kule mashinani. Asiwasikize hawa Wabunge wanaompigia kengele na ngoma. Asikize tunaomweleza mambo halisi yalivyo katika mazingara ya wananchi kule chini. Mhe. Spika, mpaka wakati huu tumekubali huyu ndiye Rais. Tunataka kusonga mbele kama Wakenya kwa sauti moja. Vile tumekubali, tunasema asidanganywe hapa na hawa Wabunge wanaompigia ngoma na kusema ooh ni kuzuri au ooh tunakusifu. Hapana. Kama Mama Mombasa, ninamwambia Rais kuwa hata hawa walimu 56,000 ambao ameajiri hawatoshi. Kwa walimu 56,000, Kaunti ya Mombasa tumepata walimu sita peke yake. Kati ya hizi free Wi-Fi hotspots 25,000, ninamweleza Rais kuwa Mombasa imepata mbili peke yake. Kama kweli anapenda ugatuzi kama alivyosema, pengine wale wanaomshauri hawamwambii vizuri. Mimi kama mama wa Kaunti ya Mombasa, ninamwambia ajibidiishe na kukazana. Asidanganywe na hawa Waheshimiwa wengine. Asante sana."
}