GET /api/v0.1/hansard/entries/1358012/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1358012,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358012/?format=api",
    "text_counter": 212,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dagoretti South, UDA",
    "speaker_title": "Hon. John Kiarie",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika, ningependa utueleze kama Mjumbe huyu wa Mombasa amekiuka Kanuni za Kudumu hapa Bungeni kwa kuwapotosha Wabunge kwa kuwaeleza kwamba kuna vituo vya kidijitali ambavyo vimebuniwa. Anajua vyema kwamba wewe mwenyewe ulituita mkutano wa kamkunji hapa na tukajadili maswala haya ya vituo hivi na ktukakubaliana kwamba ni majukumu ya Wajumbe kushirikiana na Serikali kuu kubuni vituo vya kidijitali. Pia, ninadhani kwamba huyu Mjumbe anatupotosha anapotuambia kwamba kutokana na wale walimu 56,000 ambao waliajiriwa, ni walimu sita pekee ambao wameajiriwa katika Kaunti nzima ya Mombasa."
}