GET /api/v0.1/hansard/entries/1358032/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1358032,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358032/?format=api",
    "text_counter": 232,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": null,
    "content": "zisizo na kichwa wala mguu za Building Bridges Initiative (BBI) na wanaketi mbele yetu na kutuambia vile taifa hili litaendeshwa. Mhe. Spika, deni la Kenya haliwezi kulipwa na mtu mwingine, ila sisi Wakenya. Kenya ni nchi huru ambayo inafaa kujitegemea, kuzalisha mapato yake, ajira na mambo mengine. Kwa hivyo, Rais wa Jamhuri amehakikisha kwamba minyororo na mitego iliyokuwa pale awali, ya sisi kila mara kuomba na kutegemea mataifa ya nje imeisha. Na wakati wa kulipa haya madeni ni lazima tutafute njia mbadala ndio tuweze kujikomboa. Nimesikia mheshimiwa mmoja akisema kwamba Rais anatoa ahadi nyingi sana. Ati, achague jambo moja na kulimaliza. Hata wewe mheshimiwa kwako nyumbani huli sima kila siku. Leo ni sima, kesho chapati na kesho kutwa pilau. Kwa hivyo tumuache Rais wa Jamhuri ya Kenya azunguke, aombe na atafute. Nyinyi hata leo mnapiga kelele kwa sababu ya upanzi wa miti. Tusipopanda miti mko na maneno na tukipanda miti mnaanza kusema watu wameenda kupanda. Jambo ambalo ni la…"
}