GET /api/v0.1/hansard/entries/1358037/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1358037,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358037/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Ninadhani wakiambiwa ukweli wanatafuta vijisababu visivyo na kichwa wala mguu. Nikisema hawa, ni nyinyi ambao mlikua katika Serikali iliyokua hapo awali – nyinyi ambao mliwadanganya wananchi na kuwaambia mambo ya porojo, ilhali mlikuwa mkipora mali yao. Kwanza, inafaa mrudi kwa wananchi na kuwaomba msamaha, mseme nyinyi ndio mlifanya makosa ya kupora, kufuja mali ya Wakenya na kutuletea haya matatizo. Walikuja na kifua wakisema watafanya mambo mengine kwa lazima. Leo, wanakaa mbele yetu bila aibu na kutuambia vile taifa hili litaendeshwa. Hata Hayati Emilio Mwai Kibaki alichukua miaka miwili kujenga nchi. Wewe pia kama Mbunge ulipochaguliwa huwezi fanya miujiza na kipindi cha mwaka mmoja. Kwa hivyo yale ambayo Rais alizungumzia yalikua ukweli bayana. Alizungumzia maswala ya elimu, kilimo na deni la Eurobond . Dawa ya deni ni kulipa; usidanganywe na mtu yeyote. Sisi Wakenya ndio tutalipa hilo deni na kusukuma hili gari mpaka tufike mahali ambapo patakua sawa kwa kila Mkenya. Asante sana, Mhe. Spika."
}