GET /api/v0.1/hansard/entries/1358246/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1358246,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358246/?format=api",
"text_counter": 36,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuwapa pole familia na watu wa Kholera Ward na eneo Bunge la Matungu kwa kumpoteza mheshimiwa shupavu. Bi. Spika wa Muda, nimewahi kukaa katika vikao mbalimbali na Mhe. Marehemu, ambaye licha ya ulemavu wake wa kimaumbile, alikuwa mkamilifu wa fikira na mweupe wa moyo. Yale yote aliyoweza kufanya katika eneo lake la uwakilishi, mashinani walimuenzi na kumpenda. Kukata kwake kamba ni pigo kwa demokrasia na uwakilishi wa wanawake katika uongozi wa nchi hii. Kando na viongozi wanawake ambao hawaaajibiki kimaadili na tabia zao, Mhe. Godliver alikuwa na familia. Aliwapenda watoto wake, mume wake na alipenda kanisa. Yeye ni kielelezo cha wanawake ambao wamedhihirisha ya kwamba ukimpa mwanamke nafasi, familia itakuwa imara, mwelekeo utapeanwa na matokeo yataonekana. Kule anapoenda, mkononi mwa Maulana, amwambie Mwana wa Mungu Yesu, kwamba sisi tulio hai tutaendelea na msalaba huu wa shida na mahangaiko duniani, lakini tunaamini lisilowezekana na binadamu kwa Mungu linawezekana. Godliver safari salama, tutakutana baadaye. Asante, Mhe. Spika."
}