GET /api/v0.1/hansard/entries/1358251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1358251,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358251/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kupeana ombolezi langu. Kwanza, nataka kutoa pole kwa familia ya Mhe. Godliver Omondi ambaye alikuwa Seneta katika Bunge la Kwanza la Seneti na nilikuwa ninafanya kazi na yeye kwa ukaribu sana kama rafiki. Sen. Godliver alikuwa mtu mkakamavu na mchangamfu sana. Hali yake ya afya ilikuwa sawa kabisa. Alikuwa akichangia sana mambo ya akina mama. Ninavyomuelewa Godliver hakuwepo katika ile Bunge ya Pili lakini katika Bunge ya kwanza alikuwa mkakamavu sana na aliweka mbele mambo ya akina mama na hususan mambo ya walemavu, kama alivyokuwa yeye mwenyewe. Mwenyezi Mungu amechukuwa roho yake. Kiumbe chake amekwenda nacho mwenyewe. Alimleta hapa akiwa na sababu na amemchukuwa akiwa na sababu. Sisi wote tunafaa kukubali alichopitisha Mwenyezi Mungu. Tutakachofanya ni kuwaombea waliobaki nyuma, familia yake na marafiki zake, wawe na moyo wa faraja ili waweze kupita mtihani huu kwa hivi sasa. Kilichobaki kwetu kama Bunge la Seneti, sisi ambao tunamfahamu, ni kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema walipolala wema. Asante, Bi. Spika wa Muda. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}