GET /api/v0.1/hansard/entries/1358317/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1358317,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358317/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu ya No.53(1) kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Fedha na Bajeti kuhusu Shirika la Kenya National Assurance (KNAC) ambalo liko katika hali ya upokeaji. Katika Taarifa hiyo, Kamati iangazie yafuatayo- (i) Iarifu Seneti kuhusu hali halisi ya upokeaji huo ulipofikia wakati huu, katika Shirika hilo ikieleza iwapo kumekuwa na maendeleo katika hali yao ya kifedha na shughuli zao kwa jumla. (ii) Ieleze kwa nini maskwota wanaoishi katika ardhi iliyoko Mombasa kwa Bulo Kaunti ndogo ya Nyali inayomilikiwa na Shirika hilo wameshindwa kuuziwa ardhi hiyo ilhali mwekezaji mmoja wa kibinafsi anayedai kulipa asilimia ishirini ya bei hiyo ya ununuzi alishindwa kuinunua. Asante."
}