GET /api/v0.1/hansard/entries/1358443/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1358443,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358443/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kunipa muda huu kutoa maoni yangu na kuunga mkono Hoja ambayo iko mbele yetu kuhusu Hotuba ya Rais ambayo aliitoa kwa Mabunge yote mawili. Mimi ningependa kusema mambo machache ninapoiunga mkono Hoja hii. Jambo la kwanza, Mhe. Rais aliongea kuhusu hali ngumu ya maisha ya wananchi hapa Kenya. Katika hotuba yake alikiri kuwa gharama ya maisha imepanda. Hata hivyo, yuko na mipangilio maalum ya kuimarisha hali ya maisha nchini. Baadhi ya mpangilio aliouelezea wananchi ni kuwa Serikali yake inang’ang’ana na kupunguza gharama ya chakula. Kama alivyosema Sen. (Dr.) Khalwale, Serikali ilipunguza gharama ya pembejeo kutoka shilingi elfu saba kwa begi moja hadi ikafika shilingi elfu mbili na mia tano. Wananchi wanajua ya kwamba tukipunguza bei ya pembejeo tutakuza chakula kwa wingi na gharama ya maisha itapungua. Ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja nasi wakati bei ya pembejeo iliposhuka, mvua ilinyesha na chakula kimepatikana kwa wingi. Hata sasa, wale ambao wanajua mambo ya ukulima, wakati wa mvua hii nyingi bado watu wanapanda. Tunategemea kuvuna tena chakula kingi. Kwa hivyo, tunamshukuru Mhe. Rais kwa mipangilio yake ya kusaidia mkulima wa kawaida ili chakula kiwe kingi na bei ishuke chini. Kule kwetu Tana River, hatusemi yale ambayo yameahidiwa bali tunasema yale ambayo tumeyaona sisi. Mhe. Rais katika kampeni zake wakati alipokuwa anatafuta kiti, tulipokuwa tunatembea kule, alisema, “Mimi nikiingia, nitahakikisha miradi yenu kubwa kubwa ambayo yanahusika na uzalishaji wa chakula nitayafufua ili isaidie Wakenya wote.” Alisema kuwa anataka kugeuza Kaunti ya Tana River kuwa mahali pa kutoa chakula kwa wingi na kutegemewa zaidi hapa Kenya. Sisi kule kwetu hatusemi ya kwamba ni ahadi tuu bali tumeziona jitahada zake. Hii ni kwa sababu miradi katika ile Tana and Athi Rivers Development Authority (TARDA) na Tana Delta Irrigation Project (TDIP) ambayo tuko nayo Mhe. Rais amekamilisha ahadi zake. Alianza kwa kupatiana shilingi milioni mia nne na hamsini na tukaanza pilot project . Hiyo pilot project ya ekari mia tano zimepandwa mchele. Wakati huu ukipita pale sehemu za Gamba, Sera ukielekea Hewani unaona mchele. Mahali ambapo palikuwa ni kavu bila chochote, sasa hivi unaona wananchi wanalima. Hizo ekari mia tano peke yake zimeanza kutembeza pesa sehemu hiyo kwa wingi na wananchi wanashukuru. Hii sio ahadi tu, bali sisi tumeyaona matunda ya mipangilio yake. Tena Mhe. Waziri na Katibu wa Kudumu wake wanakuja kuiangalia mradi huo mara kwa mara ili wananchi waone kwamba Serikali imejitolea kuufanikisha. Sababu ya kufufua ukuzaji wa mchele ni kwamba Kenya, kwa sasa, inatumia shilingi bilioni mia tano na arobaini kuleta chakula hapa nchini. Na ukweli ni kwamba pesa nyingi ambazo zinatumika hapo ni kuleta mafuta ya kupikia inayoitwa kwa kiingereza edible oil halafu inafuatiziwa na mchele. Wakenya huwa tunalipa shilingi bilioni sitini kuleta mchele kutoka Pakistan na nchi zingine kwa sababu hatukuzi mchele wa kutosha. Kwa hivyo, mipangilio ya Mhe. Rais katika jimbo gatuzi la Tana River imesaidia kupunguza shilingi bilioni sitini ambazo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}