GET /api/v0.1/hansard/entries/1358444/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1358444,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358444/?format=api",
    "text_counter": 234,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kenya hutumia kununua mchele kutoka Pakistan. Mchele huu ukuzwe katika jimbo gatuzi la Tana River. Katika mipangilio hiyo, Mhe. Rais alienda tena kuweka pesa katika Bura Irrigation Scheme ambayo iko hapo kwetu. Bura Irrigation Scheme iko na ekari elfu tano ambazo zinalimwa kwa chakula kwa minajili ya kuzalisha chakula. Bw. Spika, tuko na shida kwa sababu maji hayatoshi. Hii ni kwa sababu wakulima wanatumia diseli kupiga maji yaingie mashambani Gharama ya hayo maji pekee inakuwa ni shilingi milioni kumi kila mwezi. Hesabu hiyo inafika shilingi milioni mia moja na ishirini kila mwaka kuhakikisha kwamba maji yanafika katika mashamba yao. Wakati wa kampeini, Mhe. Rais wetu aliahidi kwamba ataufufua ule mradi wa kutumia gravity ili maji yawe yakiteremka kwa nguvu za kawaida. Alikuja Bura akafungua yale maji. Sasa, yanateremka bila kutumia nguvu za diseli. Ekari ambazo zimetengenezwa na kupandwa mchele nikuanzia elfu tano hadi elfu kumi na tano. Lengo letu nikufikisha ekari elfu ishirini za mchele. Kule chini tunataka kufikisha ekari thelathini. Kwa hivyo, gharama ya kuleta mchele kutoka nje ya shilingi bilioni sitini itapunguzwa na Kaunti ya Tana River itakuwa kaunti ya kutegemea kukuza mchele kwa wingi nchini Kenya. Tayari tunaona mabadiliko. Vijana wameanza kukuza mchele. Tumeona watu wengine kutoka sehemu zingine ambao wanajua faida ya ukulima wa mchele wameanza kuingia katika jimbo letu gatuzi na tunawakaribisha wote. Kuna nafasi karibu elfu thelathini za kazi ambazo zinatokea na zinaendelea kuongezeka katika sehemu yetu. Kwa hivyo, tuliposikia Mhe. Rais anaongea mipango hii ya kupunguza hali ya maisha na bei ya chakula, sisi tunajua ya kwamba ni ukweli mtupu. Watu wetu wanajua kwamba wakati lile tingatinga la TARDA linapita, wanavuna halafu wanaacha chakula wanasema wananchi ambao wanaweza waende kuchukua maanake wanachukua raundi ya kwanza na ya pili. Lakini bado kuna chakula kina baki. Watu wanaenda wanaweka magunia mengi ya mchele. Wakati ile scheme ilikuwa inafanya kazi miaka iliyopita, kulikuwa hakuna njaa. Sasa tunatarajia maisha hayo kurudi na kuwe na chakula cha kutosha hapa nchini. Tukiwa tunaongea, hatuongei maneno pekee yake, tunaongea ukweli ambao tumeuona katika jimbo gatuzi la Tana River. Jambo ambalo tungependa kulizungumzia zaidi ni kuongeza miundo misingi. Tunataka kuona barabara ambazo zinajengwa katika eneo letu ilivyoahidiwa wakati wa kampeini . Bw. Spika, hali ya maisha ambayo tunaongelea kupunguza ni kuongeza chakula na wananchi wanajua hivyo. Chakula kikiongezeka, bei zitashuka na maisha yetu yatakuwa mazuri zaidi. Kuna jambo ambalo limezungumzio nataka kulirejelea kidogo. Kenya tulienda kuomba pesa. Hatukuomba pesa kwa International Monetary Fund (IMF), Africa Development Bank ama World Bank . Tulienda kwa commercial market mahali ambapo watu wanachukua madeni kama mtu yeyote wa kawaida. Tulichukua dola bilioni mbili. Kila mtu alikuwa na wasiwasi kwamba Kenya haitalipa hizo pesa. Kenya isipolipa hizo pesa, heshima na mambo yetu mengi yataharibika. Nchi ya Ghana ilikoba katika hiyo commercial market na walishindwa kulipa, sasa nchi yao ikakuwa declared bankrupt. Sasa watu walikuwa wanajiuliza Kenya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}