GET /api/v0.1/hansard/entries/1358445/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1358445,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358445/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "itafanya nini na madeni yake. Hizo dola bilioni mbili ni shilingi billioni mia tatu na tatu. Mhe. Rais wetu amesema milioni dola mia tatu zitalipwa kufikia Decemba. Pesa hizo tayari tuko nazo. Kama watu wanasema kwamba hatusimamii uchumi vizuri, je, inawezekana mtu ambaye yuko na deni na ameambiwa kuilipa mwezi wa sita mwaka ujao anaanza kulipa mwezi hujao; miezi sita kabla tarehe ya kulipa hiyo deni? Bw. Spika, ni sawa tufanye siasa lakini pia tuseme ukweli ya kwamba tumeanza kusimamia uchumi wetu vizuri. Hizo dola mia tatu ni sawa na shilingi bilioni arobaini na tano nukta nne ( Kshs45.4 billion ) za Kenya. Pesa zipo na tuko tayari kuzilipa. Wakenya wajue kwamba mipangilio yetu ya kiuchumi inaenda vizuri. Wakati huu Okotba mwaka jana, inflation rate yetu ilikuwa asilimia 8.9. Oktoba mwaka huu, inflation rate ya Kenya ni asilimia 6.9. Hiyo ni kusema tumeshusha. Siasa tufanye lakini pia ukweli tuuseme. Oktoba hii, figures za Central Bank zinasema tumeweza kupata ushuru wa shilingi bilioni mia moja na sabini ambayo imeongezeka na asilimia 19.4 ukiunganisha mwaka uliopita na mwaka huu wakati huu wa Oktoba. Waswahili husema, “Mgala muue lakini haki yake mpe.” Mhe. Rais anafanya kazi, anaangalia huu uchumi na anapanga mambo yetu. Ni kweli tuko na shida. Ikiwa umeanzisha biashara ya tuktuk leo, ni kujifunga mkanda kwa sababu kabla matunda yatoke, kuna kule kuumia. Ikiwa unafanya kazi ya shambani na umeweka mbegu, kuna kupalilia na kulinda ndege na wanyama wasiharibu. Ule muda wa kujifunga uko lakini matunda yatakuja baadaye. Wakenya wenzangu ambao wananisikiza, kuna siasa na ukweli. Ni kweli hali ni ngumu. Hakuna mtu anakataa lakini kuna mipangilio ambayo Mhe. Rais anafuatilia ambayo itafufua uchumi wetu na ninamwamini. Akija kwetu, tumeona tofauti na ninajua maeneo ya gatuzi zingine ni tofauti ni vile yalikuwa mwaka jana na mambo yataenda vizuri. Ninawakikishia wakati mipangilio ya housing development na Universal"
}