GET /api/v0.1/hansard/entries/1358581/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1358581,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358581/?format=api",
"text_counter": 371,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kuanzia mwanzo, naunga mkono Hoja hii ya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Kenya. Ijulikane wazi, Rais mwenyewe alisema kinaga ubaga anajua kuwa maisha ni magumu lakini kuna ile mikakati ambayo imewekwa kuangazia kwamba maisha magumu ya wakenya inazingatiwa. Kwanza kabisa, bei ya pembejeo imepuguzwa kutoka Kshs7,000 mpaka Kshs2,500 ndiposa bei ya chakula iweze kupungua. Hivi sasa, sehemu zile ambazo tunategemea sana kwa hali ya ukulima wamesema kwamba wameweza kupata mazao maradufu na ni ukweli. Ukiangalia sehemu nyingi, unaona Mungu alitujalia kwa mvua na mazao yameendelea kuwa mazuri. Jambo lingine ambalo nataka kumpa Rais kongole ni alipoteuliwa kama Rais, jambo la kwanza alifanya ni kuteua majaji ambao walikuwa wamependekezwa na tume ya majaji. Hilo lilikuwa jambo zuri. Hakukomea hapo. Aliendelea na askari polisi wetu ambao hawakuwa wanajitegemea. Walipewa hela zao wenyewe waweze kuwa wao ndio wanafanya mipango kinyume ya ilivyokuwa hapo awali wakienda katika taasisi zingine za Serikali ndio waweze kupata hela zao. Hilo ni sababu la kujivunia. Sisi kutoka Kaunti ya Laikipia, ninaweza kusema peupe kimasomaso kwamba tumeona hayo mambo yakileta amani na utulivu kwa sababu usalama ulikuwa ni donda sugu. Tulikuwa kila wakati tunavamiwa na hawa majangili na wezi wa mifugo. Lakini, Serikali imejitolea. Nampongeza Rais kwa sababu alisema kuliongezwa wale polisi wa ziada. Saa hii, Kaunti ya Laikipia ina askari wa hakiba zaidi 500. Hilo ndilo jambo ambalo nasema ni afueni kwetu. Hata tukiwa na barabara au hospitali nzuri namna gani lakini kukose usalama, itakuwa kazi bure. Mimi kama Seneta wa kutoka Kaunti ya Laikipia, nampongeza Rais kwa hilo jambo zuri kwa mambo ya usalama. Akasema wazi kwamba hao wezi, wakora na majambazi wa mifugo watafuatwa mpaka kuwe na utulivu ulioko. Wale askari walioko huko; askari polisi, askari jeshi na askari wa hakiba hawatatoka, wataendelea kuishi huko huko. Bw. Spika wa Muda, jambo lingine nataka kupongeza ni, nchi hii yetu ilikuwa imekopa pesa ambazo Sen. Mungatana alisema; Eurobond. Rais alisema vizuri kabla The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}